Samahanini sana kama nitakuwa nawaudhi baadhi ya watu kwa kusema hivi lakini nadhani inatubidi tumtafute mchawi wetu maana hii haiwezekani.
Hivi kweli inawazekanaje mtu akatoa haja kubwa mahali anameandaa chakula tayari kwa kukila? Haiwezekani!
Hivi ni kwa nini tunashindwa kuelimika hata kidogo?
Tumepata shida kwa muda mrefu ya usafiri kutokana na miundombinu ya barara kuwa mibovu na kutokidhi kutokana na ukuaji wa maeneo yetu haya Mbagala na vitongoji vyake. Serikali yetu ililiona hili na hatimaye kutujengea bara bara nzuri kabisa na kwa kiasi cha asilimia kubwa tumeondokana na tatizo hili la usafiri na kama lipo basi ni lile ambalo linaikabiri Dar es Salaam nzima. Sisi na balaa letu ama upumbavu wetu tunaona ni bora kubadilisha matumizi ya bara bara hii badala ya kuwa ya magari sasa inakuwa ya 'Taka Taka' khaa! Huu si Ujinga jamani?
Nikipata bahati ya kukutana na Diamond nitamkwomba afanye remix ya wimbo wake wa MBAGALA pale anaposema "huku nyumba mbele jalala" aseme 'Bara bara mpya sasa Jalala'
Jamani Tubadilikeni

No comments:
Post a Comment