Katika safu hii ya Burudani leo hii MigoFam imeonelea iuweke kwenu muziki huu wa TAARABU ambao kwa kasi kubwa umeweza kuziteka na kuzikonga nyoyo za watu wengi wakiwemo “WAGUMU”
Migo, nikitaka kuizungumzia Taarabu basi ni lazima nitaanzia katika miaka ya Tisini kwa maana ndiyo wakati ambao nami kidogo nilikuwa na akili (matured) na kuweza kujua nini maana ya muziki.
Ni kwa kipindi hiki watanzania walipoamua kuachana na kasumba la kuabudu muziki wa nje (Kikongo na kwengineko) na kuamua kujikita moja kwa moja katika kuupenda muziki wao wa kibongo. Ndipo kipindi hiki ambapo bendi kama vile African Stars (Twanga Pepeta), TOT Band (Achimenengule), Vijana Jazz na nyinginezo zilipoudhuhirishia umma wa Kitanzania kuwa wanaweza kufanya mageuzi. Na kwa hakika walifanikiwa na hata kushika soko la muziki kwa kiasi kikubwa.
Ni kwa kipindi hikihiki pia vijana kama vile akina Juma Nature, Professor Jay, na wengineo walipoamua kuingilia kati soko la muziki na kuwateka watania wengi wakiwemo wazee katika muziki wao ambao ulibatizwa jina na kuitwa BONGO FLAVOUR.
Kwa kweli dansi na Bongo Flavour vilichukua atamu kwa kiasi kikubwa.
Kwanini basi nimeamua kuanzia kwenye muziki mwingine kabla ya kuingia moja kwa moja kwenye Taarabu?
Hii ni kwa sababu katika kipindi hikihiki wadau wa mUziki wa Taarabu akiwemo Marehemu Nasma Khamisi Kidogo (Mungu amlaze mahala pema) na wengine kama vile Malkia wa mipasho mama Khadija Kopa, Bi. Mwanahawa Ally, na wengineo wengi walipofanikiwa kuzipiga kumbo burudani zote za muziki na wao kujiweka juu baada ya kuchukua sehemu kubwa ya mashabiki wa Muziki Tanzania. Kwa hakika walifanikiwa ingawa baadaye uliporomoka kwa kiasi kikubwa na wapinzania wao Bongo Flavour na Dansi zikachukua tena nafasi.
Kanini basi nimesema MASHAUZI NAYAPA “KUBWA JUU”?
Ndani ya kipindi cha miaka hii miwili ama mitatu kuna wasanii chipukizi wengi hasa vijana wameamua kuingia kwa kasi ya ajabu katika fani hii ya muziki wa taarabu na kufanya mabadiliko makubwa kuanzia kwenye live hadi studio na kuwaacha nyuma sana wapinzani wao (Dansi na Bongo flavour). Ama kwa hakika Taarabu kwa sasa ipo juu na hawa jamaa wameamua kufanya kazi kwelikweli. Pongezi kubwa ziende kwao viongozi wa bendi hizo kwa maana bila shaka bila ya juhudi zao muziki huu usingekua hapa ulipo.
Ni kwasababu kuna COAST MODERN TAARAB ndio maana kuna OMARY TEGO, MAUA TEGO na wengineo. Ni kwa sababu ya DAR ES SALAAM MODERN TAARAB, sasa kuna HAMMER Q na wengineo uwepo wa 5STARS MODERN TAARAB ndio tukampata ISSA KIJOTI. Naamini bila ya JAHAZI la MZEE YUSUF (MFALME) ingeniwia ngumu kumuandika MADAM AISHA RAMADHANI (MASHAUZI, MASHETANI N.K) amabye kwa maana moja ama nyingine amesababisha mie NTU MME kukaa chini na kuandaa safu hii.
Madam huyu sina historia nzuri ya kujua ni lini alianza balaa hili lakini ni katika kipindi hiki kifupi amefanikiwa kuzikonga nyoyo za watu (nikiwemo mie) ipasavyo kwa namna ambavyo anawajibika awapo kazini ama kwa hakika katika fani MADAM ana MASHETANI. Ni kwa kipindi hiki pia nilifanikiwa kujua kuwa kumbe hata zile nyimbo nilizokuwa nazipenda ni yeye ndiye aliyeimba kama vile YAWENZENU MIDOMONI n.k. ebwana huyu mdada anatisha nami nampa KUBWA JUU la nguvu.
Haya niyasemayo yalijidhihirisha kwenye uzinduzi wa ALBAMU yake binafsi iliyokwenda kwa jina la (MAMA NA MWANA) yenye nyimbo gumzo ndani na nje ya jiji la Dar aliyoimba na Bimkubwa wake inayoitwa ‘MAMA NIPE HUSIA’.
AISHA ANATISHA JAMANI
NAMI NAMPA 'KUBWA JUU' (BIG UP ) LA NGUVU.

No comments:
Post a Comment