Tuesday, October 13, 2009

Niga Jei



"Ninaposema Jay ni kubwa kuliko...." YATAKA MOYO.


Huwa najaribu kuigilizia 'ze wei' anavyo 'sing' NIGGER JAY lakini najikuta nabaki kuwa ni kituko tu.

Ebwana jamaa yupo juu Kimi-'AIDIA' toka enzi za FUNGA KAZI mpaka sasa jamaa bado anaburuza katika Fani hii ya muziki wa Kufoka foka.

Kitu kikubwa kilichonifanya leo hii mimi (Pashal) kumzungumzia Nigger ingawa kwa ufupi, ni hii nyimbo ya mkali mwingine Mwana FA inayokwenda kwa jina la NAONA NAZEEKA SASA ambayo FA amewashirikisha JAY na MKONGWE SUGU. Kwa kweli ngoma imesimama.

Nigger JAY, kama ambavyo alikuwa akitambulika enzi zile za FUNGA KAZI, alitengeneza baadhi ya SEMI ambazo zinamfanya kila mwenye akili timamu afikilie huyu jamaa ana maana gani, na pia humfanya mtu anayependa kudadisi vitu kufanya hivyo. Mfano aliposema 'UKITAKA KUJUA UMUHIMU WA MATAKO, KALIA KICHWA'. Nilijaribu kumuuliza JAY alikuwa anamaanisha nini kusema hivi, kwa kweli hakupata tabu kunijibu kwani alifahamu fika jibu liko wazi ila najisumbua tu kujifikilisha, aliniambia nisimame, nami nikafanya hivyo, kisha akaniambia kalia KICHWA, kwa kweli zoezi lilikuwa gumu. Hii inaonesha wazi kuwa jamaa hufikili kabla ya kusema ama kuimba na hivi ndivyo msanii anavyotakiwa kuwa.

Sote tunajua fika hapo awali ilikuwa ngumu kwa kijana anayetoka katika familia iliyostaharabika kujihusisha na masuala ya muziki kwani ilizoeleka kuwa kila mwanamuziki (wa muziki wa kizazi kipya) ni muhuni, lakini baada ya Jay kutoka na nyimbo ya CHEMSHA BONGO,  alifanikiwa kuwateka watu wazima wengi na kuwafahamisha kuwa Muziki wa kizazi kipya si wa wahuni bali unaweza kusikilizwa ama kuimbwa na watu wa aina zote, ndipo wazazi wengi walipoamua kuwaruhusu watoto wao kuingia katika GAME na hatimaye sasa tuna wakina Jay wengi. Naye anatukumbusha kwa kusema "NILIMSHAWISHI BABA YAKO, AKAKURUHUSU UIMBE"  Aakawauliza tena "UNABISHA?"

Mi nawajibia kaka HAWABISHI na kama yupo anayebisha basi ni JEURI na atakula jeuri yake.

Hii ni mistari ya NIGGER katika NAONA NAZEEKA SASA;-

Huwezi kukwea mnazi, ili ukageme Supu
Huu ni ulimbukeni, harakati za zumbu kuku
Naona watoto wadogo, sasa wananichezea shalubu
Cheza na hili fataki, AF, Jiza na Sugu
Ah, umesahau, uzi unafuata sindano
Ni michano na tungamo, kwenye jamii mi ni mfano
Sometime nabadilika, kwa style ya T B
Ndo mana sibabaishwi na slide za Tz
CV yangu inaeleweka, kama Msondo na Sikinde
Nilimshawishi baba yako, ili akuruhusu uimbe.
Unabisha?
Ni big chata, huwezi fuata,
ni anga za maganacha, ukinifuata unanasa
Hii kama safina,wanapanda walio safi
Nchecheme nchecheme, wanagomania makapi
Ukitaka kujua Umuhimu wa Matako Kalia kichwa.

Kamua kaka.

No comments:

Post a Comment