Tunapozungumzia Afya hasa Afya bora kitu cha kwanza tutakachokitaja basi ni MDOMO kwa kuwa wenyewe ndio chanzo cha Mmeng'enyo wa chakula (Food digestion system) ambacho ndiyo kitu kikuu cha Afya ya kila kiumbe hai. Hivyo basi endapo tutazungumzia AFYA bila kugusia MDOMO tutakua hatujatenda haki.
Mdomo ni sekta nyeti katika afya ya mwanadamu hivyo basi ili kuiweka afya yetu katika hali nzuri inatupasa kuwa waangalifu juu ya utunzaji wa kiungo hiki muhimu sana kwetu. ni lazima tufahamu kuwa Usafi ndiyo kitu kikubwa cha kuzingatiwa katika swala zima la Afya na kwa kuwa tunazungumzia MDOMO basi nitapenda kuzungumzia usafi wa MDOMO.
Swala la usafi wa mdomo si swala la hiari hata kidogo ni swala la lazima kwa maana tusipokuwa wasafi midomoni mwetu tutakuwa na hatari kubwa kiafya ikizingatiwa kuwa MDOMO ni chanzo cha Mmeng'enyo wa chakula. pia ninaamini kwamba bila ya kufahamu mazingira ya nyumba yako itakuwia vigumu kuyaweka mazingira hayo katika hali ya USAFI ndiyo maana leo nimeamua kuyaweka mazingira ya MDOMO wazi ili kukuwezesha kuyafamu na kuyatunza vyema.
SASA NI MARUFUKU WATU KUNUKA MIDOMO kwani ni kero kwako na wengine pia.

No comments:
Post a Comment