Thursday, October 29, 2009

Kwa Mtindo Huu 2tafika Kweli!?

Wakati Viongozi na Raia kwa pamoja tunalilia hali nzuri ya kimaisha bado kuna vitu ambavyo labda havihisiwi kuwa ni chanzo cha hali mbaya hasa kiuchumi au kama vinafahamika hivyo sijui vinachukuliwa uzito wa kiasi gani.


Kituoni Gongo la Mboto

Wanafunzi wakisuburu Usafiri ili wawahi kwenda shule


Usafiri kwetu watu tuishio maeneo
ya Gongo la Mboto na vitongoji vyake bado ni kero pamoja na jitihada za wadau wa sekta hiyo nyeti kujitahidi kujitolea mabasi yao makubwa kwa ajili ya kutunusuru.

Kwa uchunguzi uliofanywa na wakazi wengi wa maeneo hayo unasema kuwa BARABARA ndio chanzo kikubwa cha tatizo hili linalopelekea wanafunzi kuchelewa mashuleni na wafanyakazi kuchelewa makazini.

Tunaelewa fika kwamba maendeleo ya kila Taifa huletwa na jitihada za watu wenyewe makazini, sasa swali lanakuja; Ni jinsi gani utaonesha jitihada za kazi ukiwa umeshachoka kwa kugombania usafiri, ushagombana na watu mbalimbali kwenye daladala na kusababisha pengine kuumia? Ushachelewa kazini na kukosa baadhi ya kazi ambazo tayari zimewahiwa na waliowahi? Wapi utapata 'Mudi' ya kazi kwa mtindo huu? ni Vipi wanafunzi watafaulu mitihani yao ikiwa kabla ya kupambana na mitihani hiyo wanapambana na Usafiri kwanza?

Kituoni Gongo la Mboto

Wanafunzi wakivizia dirisha ili wapite na kuweza kuwahi shuleni.

Kwa kweli tukifanya mchezo hatutafika tunapopataka.


Tunaandaa makala maalum ya Shida ya USAFIRI, kama utakua na lako la kutuambia usisite kufanya hivyo kupitia (pashalonline@yahoo.com).

No comments:

Post a Comment