Ama kwa hakika gharika li njiani laja ni likifika halitamuacha mtu kwa maana likiona chanzo huwa halimchagui mtu mmoja.
Inasikitisha sana kuona kwamba wakati Watanzania tukipigania maendeleo ya maeneo ama ya nchi yeo, bado kuna watu ambao wapo katika zama za UJIMA (wanapenda kukaa watupu bila nguo) mpaka sasa.
Sina maana mbaya hata kidogo katika hili. Ukweli ni kwamba inasikitisha sana. Inasikitisha kuona mambo kama haya yanafanyika sehemu ambayo watu wa rika na nyadhifa tofauti wanaishi.

Inasikitisha kuona watoto zetu nao wapo mstari wa mbele kushuhudia haya.
Itasikitisha kumchapa/kumuadhibu mtoto eti kwa nini ameenda kushuhudia wakati na wewe mzazi upo katikati ukifurahia haya.
Ni wapi mwendo wetu? Ni wapi mwisho wetu?
Labda bado hamjanipata vyema..... Tazama hii!!!
Mdada akionyesha sehemu zake za faragha wakati wa sherehe mtaani kwetu huku akishuhudiwa na watu wengi wakiwemo watoto wadogo.
Naogopa kusema kitu juu ya mdada huyu kwa maana pengine ni mtoto wa mtu fulani anayeheshimika mtaani hapa ama ni mtu aliyetolewa mbali ili kuja kuwaharibu watoto wetu mtaani. Lakini swali langu linabaki hapa:-
Mko wapi nyie tuliopanga foleni siku ya Tarehe ishirini na tano mwezi wa kumi (25/10/2009) na kuwachagua mtuongozee mitaa yetu? Je, hii sio miongoni mwa kazi zenu kuhakikisha Tabia na mienendo ya jamii inayokuzunguka iko sawa?
Labda nisiwahukumu hawa Wenyeviti wa serikali za mitaa bali nitupe lawama pia kwa wenye shughuli zao ambao kwa makusudi uamua kuwaarika wacheza uchi hawa kumwaga radhi mitaani kwetu.
Nadhani huu ni wakati muafaka kwa akina MARIAM MIGOMBA, DINA na wenzao pia kuwachana LAIVU watu wa namna hii kwenye vipindi vyao kama vile MCHARUKO, SASAMBU na vinginevyo kwa maana ndivyo ambavyo kwa namna moja ama nyingine ndivyo vipendwavyo sana na akina dada/mama
Ama kwa hakika huu ni MCHARUKO.

No comments:
Post a Comment