Friday, July 23, 2010

KILIMO KWANZA

Tunapoamua kumuunga mkono Mheshimiwa Rais katika vitu mbalimbali asemavyo basi tumuunge mkono kwa vitendo na si kwa maneno. kwa kulitambua hili, kila mmoja wetu na ajipangie japo siku moja katika Juma ama Mwezi ahudhurie sehemu ama alifanikishe jambo ambalo Mheshimiwa analipigania, Huku ndio kumuunga mkono kunakotakiwa.

Mheshimiwa Rais amekuja na mbiu isemayo 'KILIMO KWANZA' hakua na maana mbaya hata kidogo, lengo lake ni kila mmoja wetu atakaye kujikwamua kiuchumi basi afikilie kwanza ni nini UTI wa mgongo wa Taifa letu na kisha baada ya kupata jibu ambalo ni KILIMO basi aanzie huko (kwenye kilimo) ili mambo mengine yafuate.

Kwa kulizingatia hili, Mimi (Migomba) huelekea shambani japo mara moja kila baada ya wiki mbili kufanya mambo yanayotakiwa huko ili kujikwamua kimaisha.

Hapa nikiwa kwenye kipande changu kidogo cha shamba kilichopo Chanika nikimuunga mkono Mheshimiwa Rais katika lile la KILIMO KWANZA.

wakati wewe unauziwa kipande kidogo sana cha Muhogo kwa kiasi cha pesa kisichopungua shilingi 100, mimi mwenzio 'najisevia' tu tena 'bwerere'.


Ni baada ya kazi ya muda fulani hivi sasa nimepumzika sehemu najipatia PANDE la KASAVA.


Najua fika kuna watu ambao wananionea DONGE lakini si kosa langu, ni maamuzi tu haya. Najua pia kuna watu ambao ambao wanatamani kupata maeneo ya japo kujipandia mchicha tu lakini hawayapati, sitaki kuwapa pole watu hawa kani pia yawezekana ni uzembe. Hebu tujiulize hivi kweli sisi sote tumezaliwa Amana, Muhimbili, Temeke, Mwananyamala ama sehemu nyinginezo za jiji la Dar es Salaam na tunaishi hukuhuku maisha yetu yote? Hivi kweli sisi hatuna makwetu kwenye maeneo mengi ya wazi? Hapa tutadanganyana tu bwana, hebu tuchukue maamuzi yaliyosahihi, tuwaachie wavivu tu waidshi Dar sisi twendeni home japo kwa mwaka mmoja tu, HAKI YA MUNGU tukirudi tutakuwa wapya na watatuheshimu.

KUMBUKENI 'HAKUNA AJIJUAYE ASIYEJUA KWAO'

No comments:

Post a Comment