Kuna maswali ambayo sisi Watanzania tunapaswa kujiuliza kabla hatujatafuta wakumfunga Paka Kengere. Hivi ni nani alaumiwe kati ya wamiliki na waendeshaji wa wa vyombo ama shirika hili la usafirishaji (RAILWAY)
Hiki ni chombo muhimu sana katika uchumi na hata kijamii kwa kuwa ndicho kitegemewacho na watu wengi toka mikoa ya kanda ya ziwa na mikoa ya kati ya nchi yetu. Sitaki kuilaumu Serikali kwa kuwa labda upeo wangu ni mdogo katika haya, lakini je, ninapaswa kunyamaza? Sijui.
Leo tarehe 06/09/2009 treni ya reli ya kati iliyokuwa ikitokea Mwanza kuja Dar es Salaam imekwama Pugu, na kusababisha watu kupata hadha ya usafiri iliyosababisha watafute usafiri wa daladala. Je, niendelee kunyamaza? Aaah inakera sana na hasa ukizingatia inanihusu kwa namna moja ama nyingine.
Swali linabaki kwenu wadau, Je, Kimtindo huu 2tafika?



No comments:
Post a Comment