Kama tungizungumzia burudani, itakuwa 'c o ishu' endapo tutaacha kuwataja wawezeshaji wa burudani hizo kuwepo. katika safu yangu hii mpya ningependa kuanza na mtangazaji huyu mahili wa vipindi tofauti Redioni na hata Runingani, huyu c mwingine bali ni,
MaMi.
MaMi.

Mariam wa Migomba Mama wa 3-0, mama wa Micheruko, mamaa wa mambo ya pwani kama wapendavyo kumwita wapenzi wa mwanamama huyu mahili wa TBC FM na TBC TV. Umahili wake huu hasa katika kujishebedua akiwa hewani na kujua nini afanyacho na kipi wapenzi wake wanataka toka kwake, kumesababisha watu wamfananishe na aliyekuwa mtangazaji muhasisi wa Redio Clouds Fm wa kipindi kama chake cha Muziki wa mwambao na vipindi vinginevyo kikiwemo kipindi cha AFRICA BAMBATAA, marehemu AMINA CHIFUPA, Mwenyezi Mungu amrehemu.
Ukimsikiliza mara ya kwanza utatamiani umsikilize tena kwa mara nyingine, nyingine na nyingine na hata nyingine. Ama kwa hakika anastahili pongezi mwanamama huyu.
Mpenzi mdau, ili kuboresha blog yetu ninahitaji maoni toka kwako hasa kuhusu mambo mbalimbali ya kijamii, kumbuka hii ni Blog yetu.
Tuma maoni yako kupitia: pashalonline@yahoo.com

No comments:
Post a Comment