Sunday, September 13, 2009

MJOMBA

Mwanalugha  (Mrisho Mpoto) akiwajibika katika viwanja vya Biafra kwenye Kongamano la
TUWAJARI WENZETU
 
Kama itatokea ukanikuta usingizini, kisha ukanikurupusha ghafla, tena kwa bakora na kuniuliza NI NANI MSANII Ninayejisikia fahari kusikiliza maneno yake ama nimpendaye na ninatamani 'niwe kama au zaidi yake, Basi nami nitakujibu tena kwa uhakika wa 100% ni MPOTO
Naam, Mrisho Mpoto ni msanii ambaye ametokea kupendwa na watu wengi sana hasa kutokana na staili yake ya kuimba kwa kutumia mtindo wa MAJIGAMBO na kutohoa baadhi ya maneno yatokanayo 'na vitendawili, Semi na hata Misamiati. Ama kwa kila mpenda Lugha yetu hii ya Kiswahili atalazimika kumpenda Mpoto kwa namna anavyoiwakilisha vyema katika jamii yetu hii ya Kiswahili na hata kwa wasiotumia Kiswahili. Anawafanya watu wajue kuwa Kiswahili bado kipo hai na si kama wadhaniavyo wengi wapendao lugha ngeni kama Kiingereza na lugha nyinginezo na kuisahau lugha yetu hii iliyokamilika na yenye msisimko wa aina yake kwa kila aizungumzaye. 
Mpoto, anawaambia watu hawa kuwa;
"KUFUMBATIA MAJI KAMA JIWE, NI UJINGA
Ni kweli kwamba sote tunajua kuwa maji ni kimiminika je, ni vipi twataka kuyakumbatia, hivi ni kweli hatuna namna nyingine ya kuyahifadhi? Mimi naitafsiri Maji ni kama lugha ngeni na Jiwe ni kama Lugha yetu asilia (Kiswahili). Basi yatupasa sisi kuizingatia yenyewe ili tusifananishwe na WAJINGA.
Ukipata bahati ya kumuona Mpoto akiwa Stejini akiigiza, basi ni lazima utamkubali na kusema ama kwa hakika hakuna msanii wa maigizo kama huyu. Si stejini tu bali hata kwenye baadhi ya filam ambazo ameshiriki utatamani kipande chake tu ndiyo kiwe kinaonekana muda wote, kama unabisha tafuta Kindergarten utakubaliana nami.
Naomba nieleweke vyema, sina maana ya kuwa hakuna wasanii wengine niwapendao, La hasha, wapo wengi mno lakini kwa leo ni huyu MJOMBA. 
HONGERA.

No comments:

Post a Comment