Thursday, December 15, 2011

KUKATIKA KWA MPINI SIO ........ (WEMA)

Yeah wadau wa MigoFam leo nimeamua kumtupa kwenu binti wa Mzee Abraham Sepetu (Wema) kwakua ni msichana ambaye amefanikiwa kuwa gumzo sana midomoni mwa watu kutokana na kuandikwa sana katika vyombo vya Habari hususan Magazeti. Simleti kwenu kwa maana nataka nami niwe miongoni mwa waandishi wake (Wema). La hasha. Bali nataka kumpa pole na kumtakia mambo kadhaa ambayo pengine yatamweka ama kumrudisha katika heshima ambayo mimi naamini kuwa anayo ila watu walijaribu kuiteketeza tu kwa hira zao binafsi.

Wema Abraham Sepetu


1) WEWE NI MZURI - Nataka dada yangu ufahamu kuwa wewe ni mzuri na pengine zaidi ya hao wenzio ingawa sisemi kuwa wao ni wabaya.

2) UNA VIPAJI - Hili halipingiki kwani kila mtu anafahamu fika kuwa sababu ya wewe kuwa ulipo ni kutokana na vipaji ambavyo Mungu amekutunuku achilia mbali mambo yale ya mavazi hiki cha Uigizaji kinakuweka juu zaidi.

2) UNAPENDWA SANA - Kutokana na sababu nilizozitaja hapo juu watu wengi sana wanakupenda.

3) UNACHUKIWA SANA - Kutokana na sababu hizo tatu za hapo juu watu wengi pia wanakuchukia.

WEMA.
Ukiyagundua haya na kuyafanyia kazi utakuwa katika wakati mzuri sana na hakuna kitakachokusumbua katika maisha yako kwa maana safari yako ya kimaisha bado ni ndefu mno na ni ngumu mno.

Naomba nikukumbushe kitu kimoja: Miaka kadhaa iliyopita kulikuwa na skendo moja babkubwa lililomkumbaga aliyekua (Sina hakika kama bado yupo katika tasnia) muigizaji maarufu (Christina aka Sinta) na mwanamuziki maarufu ambaye naye kwa wakati huo alikua juu sana (Sir Juma Nature). Nisingependa kuingia ndani hasa kutokana na kisa cha hawa watu ila nataka nawe uchukulie mfano wao kwa maana Sinta ni kama wewe na Nature ni kama Diamond katika mkasa huu. Hii ni kama REMIX.

 Wema na Diamond wakati wa mapenzi yao
 Aliyekua muigizaji wa Kaole - Sinta


Kibla Sir Juma Nature


Najua ya kuwa ulimpenda sana Bw. Mdogo sana Diamond lakini haupaswi kulia ovyo na kujidhalilisha mbele za watu eti ndo utamfanya akuonee huruma, si kweli bali badala yake atazidi kukuona kuwa unampenda sana na kukufanya atakavyo. Amini nakwambia anaweza kukurudia na kukutema tena. Unachotakiwa ni kukaa na kuiga mfano wa dada Sinta wa kuanza maisha mapya na sio kukurupuka na kuanza mahusiano mapya na mtu yeyote eti sababu ni maarufu au ana fedha. Dada amini ya kuwa Mpenzi wako wa kweli na wa kudumu na hata wa kumpatia watoto, yupo ni kiasi cha kusubiri tu.

MAOMBI YANGU KWAKO
Sikuombea eti iwe ndio jamaa awe amekumwaga kiukweli kweli. La hasha. Ila kama itakuwa hivyo basi kama nilivyotangulia kusema, wako yupo anakusubiri ngoja ajitokeze naamini utafurahi mwenyewe. Wema wewe ni MZURI SANA.


Rahim R. Migomba

No comments:

Post a Comment