Thursday, May 28, 2009

UUUhhhhh! Kichwa kinauma. Anyway,
Niko kwa ofic napablishi mai blogu ili kuwapa rubudani ninyi wadau.
Yeah, ni mimi PashalOnline (Baba Rahmaritah)
Hahahahaaa! Yeah ni baba yangu mzazi
Dr. Ridhaa Migomba 'Mzee wa Sunna' (Kushoto) akidickac ki2 na
Babu yangu Mzee Shomary Chugulo (Kulia),
siku ambayo nilikuwa nakabidhiwa JIKO.

Naam! Nimekubali, ... Kumuoa, ...... Binti yako, ... Fauzia Bint Edward, ......
Haya ni maneno ambayo yalikuwa yakitamkika
toka kinywani mwangu siku hiyo ya
tarehe 29/07/2006 maeneo ya Maweni, Mji Mwema, Kigamboni.
Hii ilikuwa ni wakati tukielekea 'ukweni' tayari kwa kukabidhiwa
majukumu. Kushoto ni Ustadh Mosi na kulia ni best man wangu
Rajab Kautipe. Moyo Pwapwapwaaa!?
Ilikuwa ni wiki moja kabla ya ndoa, mimi (Pashal Migomba)
nikiongoza ndugu zangu tulitinga katika
Ukumbi wa Balakuda Maweni Mji Mwema
tulipoalikwa na wakwe zangu (watarajiwa kwa wakati huo)
katika hafla fupi ya kumuaga binti yao.
Baada ya kukabidhiwa 'Jiko' langu kilichofuata ni kujisherehesha.
Yeah! ilikuwa ni ucku wa aina yake ambao nilitamani usiishe.
Ilikuwa ni sherehe ndogo lakini kwangu ni kama kubwa. Nilifurahi sana.
Ule wakati muafaka na muhimu katika sherehe ambao
pengine wengine uhudhuria sherehe mbalimbali kwa ajiri ya wakati huu
ndo umefika, Naam wakati wa maakuli.
Mimi na wife wangu tuliuongoza
msafara wa kuelekea kijiji ambacho Msosi ulipatikana.
Sikumbuki nilikuwa nafanya nini hapa ila nakumbuka kila nilichokuwa nafanya
kilikuwa ni amri toka kwa Mr. Kondo (MC) aliyekuwa akisherehesha sherehe hiyo.
Yaani tulikuwa kama mazuzu.

Na kwa pete hii, ninakuoa, ... huko mbele sikuweza kujua alikuwa akisemaje Bob Ludala ambaye alikuwa akisikika toka katika spika za Muziki uliokuwa ukituburudisha siku hiyo huku tendo la kupachikana PETE likiendelea.

Bonge la UTAM. Kushoto ni Matroni wa mke wangu
Bi. Veronica na kulia ni Bw. Rajab Kautipe Best man wangu.

No comments:

Post a Comment